IQNA

Watumiaji wa Mitandao ya Kijamii wamkosoa  Qari wa Kuwait  anayeunga mkono vita vya Trump dhidi ya Iran

19:30 - April 03, 2026
Habari ID: 3482115
IQNA – Qari wa Qur’ani Tukufu kutoka Kuwait ameunga  mkono shambulio vita haramu vya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuibua hasira kubwa na ukosoaji kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Mashary Rashid al‑Afasi hivi karibuni ameonyesha uungaji mkono wake kwa uchokozi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Akinukuu Ikulu ya Marekani (White House) na kuunga mkono vita vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, aliandika katika moja ya mitandao ya kijamii: “Trump amefungua milango ya jahannamu juu ya Iran.”

Msimamo wake umepelekea tovuti maarufu zaidi duniani ya Qur’ani kuondoa kisomo cha al‑Afasi. Hatua hiyo ya tovuti ilipokelewa kwa shangwe na kuungwa mkono na Waislamu wengi duniani.

Hapo awali al‑Afasi alikuwa ameonyesha mshikamano wake na muungano wa Saudia na Imarati kwa kuvaa sare ya rubani wakati wa mashambulizi dhidi ya Yemen. Lakini safari hii, kuunga mkono vita dhidi ya Iran ambavyo vinaendelezwa  vya Trump, ambaye ni mhalifu mwenye chuki dhidi ya Uislamu, kwa kushirikiana na utawala wa Kizayuni, kumezua wimbi kubwa la hasira miongoni mwa Waislamu.

Sauti ya al‑Afasi bado ipo katika kumbukumbu (archive) ya tovuti ya Quran.com, lakini jina lake halionekani tena katika orodha ya wasomaji unapochagua msomaji wa kusikiliza.

Mtumiaji mmoja kutoka Iraq aliandika akiunga mkono kuondolewa kwa jina lake akisema: “Kuunga mkono madhalimu ni mstari mwekundu, hata kama msomaji huyo ni mashuhuri duniani.”

Sheikh Azhar Nasser, mwanazuoni kutoka Iraq, pia aliandika: “Hii ni dalili kwamba mtu anaweza kuwa msomaji mashuhuri wa Qur’ani duniani, lakini wakati huohuo akawa mtu mwenye tabia mbaya sana.”

Mwanaharakati mwingine wa Kiislamu aliyejitambulisha kama SG aliandika: “Imepokewa kwamba Mtume (SAW) amesema: ‘Kutakuja watu katika umma wangu watakaosoma Qur’ani kwa sauti nzuri sana, lakini haitapita koo zao. Watatoka katika dini kama mshale unaopita kwenye shabaha bila kubaki ndani, na hawatarudi tena. Hao ndio viumbe wabaya zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu.’”

Mtumiaji wa mitandao ya kijamii Yamina Sayed aliandika: “Kusoma Qur’ani na kuitekeleza ni mambo mawili tofauti; watu kama hawa hawafuati maadili ya Uislamu ipasavyo.”

Mtumiaji kutoka India, Sadaf Afarin Salaf, naye aliandika: “Mfano wa wale waliopewa Taurati kisha wakashindwa kuitekeleza ni kama punda anayebeba vitabu.”

Mtumiaji mwingine wa India, Irfan Rao, aliandika: “Kumbukeni kwamba Mtume (SAW) alisema kuhusu Khawarij kwamba watasoma Qur’ani kwa sauti nzuri sana.”

4344074

captcha